NIMSHUKURU Mungu kwa kuniweka salama na kuja kuzungumza nanyi kwa njia hii ya maandishi.
Mchakato wa uchuguzi wa viongozi kuanzia rais, wabunge na madiwani kwa njia ya kidemokrasia hufanywa kwa njia ya kupiga kura.Huu ndiyo wakati ambao kila mwananchi mwenye umri wa miaka 18 na zaidi hushiriki kuchagua viongozi wa kushika madaraka ya dola na uakilishi kwa kipindi cha miaka 5 kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ili mtu aweze kupiga kura sheria inaelekeza kwamba, ni lazima awe amejiandikisha na kupewa kitambulisho kinachomuwezesha kutambulika kwamba ni mpiga kura halali wa kituo husika.Kuhusu uteuzi wa wagombea kupitia vyama vya siasa vilivyosajiliwa, ieleweke…
Jaji Damian Lubuva.
NIMSHUKURU Mungu kwa kuniweka salama na kuja kuzungumza nanyi kwa njia hii ya maandishi.Mchakato wa uchuguzi wa viongozi kuanzia rais, wabunge na madiwani kwa njia ya kidemokrasia hufanywa kwa njia ya kupiga kura.Huu ndiyo wakati ambao kila mwananchi mwenye umri wa miaka 18 na zaidi hushiriki kuchagua viongozi wa kushika madaraka ya dola na uakilishi kwa kipindi cha miaka 5 kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ili mtu aweze kupiga kura sheria inaelekeza kwamba, ni lazima awe amejiandikisha na kupewa kitambulisho kinachomuwezesha kutambulika kwamba ni mpiga kura halali wa kituo husika.Kuhusu uteuzi wa wagombea kupitia vyama vya siasa vilivyosajiliwa, ieleweke kwamba hufanywa baada ya wagombea kuchukuwa, kujaza na kurejesha fomu za kuomba vyama vyao kuwapendekeza wagombee kwa tiketi ya vyama vyao.
Hatua hii ni muhimu kwa sababu vyama huwashindanisha wanachama wao, ili kumpata mgombea aliye bora.
Wakati wa mchakato huu vyama vya siasa kwa kutumia kanuni za katiba zao,vina wajibu wa kuakikisha wagombea au mawakala wao hawakiuki sheria za nchi, hasa kwa kujihusisha na rushwa.
Wakati huu ndiyo wa kumtathmini mgombea, kama anaweza kuleta maendeleo yanayozingatia mhimili wa amani, usalama na utulivu kama mtaji wa maendeleo ya jamii anayoomba kupewa fursa ya kuiongoza.
Ndugu zangu, huko tuendako ni wakati wa kampeni ni wakati wa ushawishi wa nguvu ya hoja na sera wenye lengo la kuomba kuchaguliwa na wapiga kura.Kwa sababu kura pekee ndiyo inayotoa ridhaa kwa mgombea kushika madaraka ya dola au uwakilishaji katika mamlaka za maamuzi, nawaomba wapiga kura kutomchagua mtoa rushwa kwani atatuumiza akipata madaraka.
Inafahamika kuwa kampeni na ushawishi humwezesha mpiga kura kuwafahamu wagombea, vyama vyao na sera zao na yule mchafu hugundulika wakati huo, hivyo tuwe macho wakati ukifika.
Sheria inatoa uhuru wa kampeni kufanywa nyumba kwa nyumba, kujitangaza kupitia vyombo vya habari, kubandika matangazo au mabango, mikutano ya hadhara n.k lakini inakataza rushwa na udhalilishaji.
Katika hatua hii ni muhimu kila mgombea afahamu na kuepuka makosa yafuatayo:- Kufanya kampeni kabla au baada ya muda ulioruhusiwa, kutumia lugha ya matusi, kashfa au uongo katika kampeni na ushawishi, kueneza uongo dhidi ya mgombea wa chama chochote, kuwatisha, kuwabughudhi au kuwazuia wapiga kura, kufanya fujo au vurugu.
Mgombea na mpiga kura ni marufuku kutoa au kupokea rushwa n.k. Kumbuka mtu akitenda kosa, sheria itachukua mkondo wake na kila mgombea anao wajibu wa kuwaelimisha wafuasi wake umuhimu wa amani, usalama na utulivu kabla na baada ya uchaguzi.
Pia ni wajibu wetu kutambua kwamba wakati wa kampeni ukifika ni kosa kuondoa, kuchana au kubandua matangazo ya wagombea pia ni kosa kuandika maneno mengine kwenye matangazo hayo na ni kosa kubandika matangazo katika maeneo au sehemu zisizo ruhusiwa au juu ya tangazo la mgombea mwingine (kuliziba).
Kwa upande wa polisi nao watambue kuwa wao ni chombo cha umma, hakitumikii chama chochote cha siasa bali ni chombo kinacho wajibika kutenda kwa haki na usawa bila upendeleo katika mchakato mzima wa uchaguzi.
Pamoja na wajibu wa kulinda amani na usalama wa raia wote, katika kipindi cha uchaguzi utekelezaji wa majukumu unaweka mkazo katika mambo kama vile kuhakikisha mikutano ya kampeni inafanyika na kumalizika salama, ihakikishe kwamba zoezi la upigaji kura linaenda sawa, bila vikwazo au bughudha na kujua kwamba vifaa vya kupiga kura viko salama yaani haviibiwi wala kughushiwa na watu wenye nia mbaya .
Polisi wana wajibu wa kuhakikisha mchakato wa kupiga kura, kuhesabiwa na kutangazwa matokeo unakuwa huru na haki.Wananchi wanapaswa kujua kwamba kisingizio cha kutojua sheria iliyovunjwa, siyo sababu ya kutokamatwa na kushtakiwa.Hivyo kutii sheria na taratibu za uchaguzi ni wajibu wa kila mpiga kura. Elimu hii ilipaswa kutolewa kwa wapiga kura lakini sikuona inatolewa huku tukikaribia kuanza kampeni.
Ni lazima Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini ya Jaji Damian Lubuva kuona itafanya nini ili watu waelimike kuhusu uchaguzi, vinginevyo ni vurugu.Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
No comments:
Post a Comment