Jengo la mamlaka ya maji wilayani kibondo lililoko katika chanzo cha
maji Mugoboka
(picha na James Jovin )
Tatizo la maji wilayani
kibondo mkoani kigoma linategemea kuisha hivi karibuni baada ya halmashauri ya
wilaya hiyo kutumia zaidi ya milioni 100 kupeleka umeme katika kijiji cha
Mugoboka ambapo pampu ya umeme tayari
imefungwa ili kutatua tatizo la maji wilayani humo
Ameyasema hayo mkuu wa wilaya
ya kibondo bw Venance Mwamoto wakati alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari
akiwa ofisini kwake juu ya ukosefu wa maji uliodumu kwa zaidi ya wiki tatu sasa
Amesema kuwa ukosefu wa maji
unatokana na malekebisho makubwa ambayo yanafanyika katika chanzo cha mto
mgoboka ikiwa ni pamoja na kubadilisha mabomba yanayopitisha maji kutokana na
yale ya zamani kushindwa kuhimili nguvu za mashine mpya iliyowekwa kwa ajili ya
kusukuma maji
Aidha zaidi ya shilingi milioni 200 zimetumika katika kupanua
na kuongeza miundo mbinu ya maji wilayani kibondo mkoani kigoma ikiwa ni pamoja
na kusogeza huduma ya maji kwa wakazi wengi zaidi
Meneja wa maji wilayani
kibondo bw Matwiga Tandale amesema kuwa tayari mpango huo umeanza kufanyiwa
kazi ambapo tayari
umewekwa katika bajeti ya
mwaka huu inayoendelea kufanyiwa kazi jijini dare s salaam
Amesema kuwa katika kuboresha
huduma ya maji visima vyenye pampu ya mkono vitabadilishwa na kuweka pampu ya
umeme ili kurahisisha upatikanaji wa maji pamoja na kuboresha miundo mbinu kwa
ujumla
Aidha bwa Tandale amesema pia
wameomba fedha shilingi million 48 kwa ajiri ya kujengea uwezo wa kununua units
za umeme pindi watakapoanza kutumia chanzo cha mgoboka ambacho kitakuwa
kikitumia pampu ya umeme
Mchakato wa kufunga pampu
hiyo yenye uwezo wa kusukuma maji lita milion 3 na laki 9 kwa siku bado
unaendelea katika chanzo cha maji cha mgoboka ambapo itaanza kutumika mwishoni
mwa mwezi mei
Mabomba ya maji yakiwa tayari kwa ajili
ya kuanza mchakato wa kubadilisha yale ya zamani ambayo hayawezi kuhimili
ukubwa wa mashine mpya yenye uwezo wa kusukuma maji mara tatu ya ile iliyokuwepo (picha na James Jovin)
Kutokana na miundo mbinu hiyo ya maji kuboreshwa zaidi ya
wakazi elfu 10,000 wilayani kibondo mkoani kigoma wanatarajia kupata huduma ya
maji baada ya idara hiyo kuagiza pampu ya maji yenye uwezo wa kusukuma lita milion 3 na laki 9 za maji kwa siku
Mhandisi wa maji wilayani kibondo bw Joseph Njela ameyasema
hayo alipokuwa akiongea na radio kwizera akiwa ofisin kwake
Bw Nzela amesema kuwa
pampu ya maji iliyopo kwa hivi sasa inauwezo wa kusukuma maji lita
milioni 1 na laki 3 na inauwezo wa kuhudumia watu elfu 17 hivyo baada ya
kufunga pampu hiyo mpya wataongeza watumiaji
wengine zaidi ya elfu 10
Aidha amesema kuwa halmashauri imetumia zaidi ya milioni 114
kupeleka umeme katika chanzo cha maji cha Mugoboka ikiwa ni ulefu wa zaidi ya
kilometa 3.2 kwa ajili ya kuanza
kusukuma maji kwa kutumia umeme na kinachosubiriwa kwa hivi sasa ni pampu hiyo
ambayo inategemewa kuwasili mwishoni mwa mwezi huu
Mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance mwamoto akiwa
anajaribu mtambo mpya wa kusukuma maji utakaoanza kufanya kazi hivi karibuni
mtambo huo unauwezo wa kusukuma maji lita zaidi ya milioni 3 kwa siku (picha na James Jovin)
Katika kuboresha upatikanaji
wa maji katika chanzo cha mto Mugoboka miundo mbinu imeboreshwa ikiwa ni pamoja
na kuhamasisha wananchi kuacha kulima katika vyanzo vya maji ili kuboresha
mazingira pamoja na kuongeza chemi chemi za maji
Mkuu wa wilaya ya kibondo bw
Venance Mwamoto akiwa ameingia kwa nguvu mpya pamoja na slogani yake ya kazi
kwanza maneno badae amesaidia sana katika kuhakikisha miundo mbinu hiyo ya maji
inatengenezwa haraka iwezekanavyo ambapo amekuwa akifika mara nyingi katika
chanzo hicho cha maji ili kuhamasisha mafundi kufanya kazi hiyo haraka
iwezekanavyo.
Mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance
Mwamoto akifuatilia hatua kwa hatua ujenzi wa miundo mbinu ya maji katika
chanzo cha mto mgoboka (picha na James Jovin)
No comments:
Post a Comment