Pages

Tuesday, September 4, 2012

maoni ya katiba wanawake waendelea kuwa wachache

baadhi ya wananchi wilayani kibondo wakiwa wamepanga msitari tayari kwa kutoa maoni yao kwa tume ya mabadiliko ya katiba (picha na james jovin)


KIBONDO
Jeshi la polisi kote nchini limetakiwa kufanya kazi zake kama maadili ya jeshi hilo yanavyosema na si kwenda kinyume  kwa kutumia nguvu nyingi na siraha za moto kitu kinachosababisha jeshi hilo  kuwa chanzo cha vurugu miongoni mwa jamii

Wito huo umetolewa na bi Frola  Chiristopher mwanamke pekee aliyejitokeza kutoa maoni  wakati  tume ya mabadiliko ya katiba  ilipokuwa ikikusanya maoni katika kata ya kitahana wilayani kibondo

Bi Christopher pamoja na mambo mengine amesema kuwa ni vyema katika katiba mpya ijayo jeshi hilo lidhibitiwe ili kulinda maadili ya jeshi hilo na usalama wa raia kwa ujumla

Kwa upande wake mwenyekiti wa tume hiyo bi Mwatumu Malale  amesema kuwa kukusanya maoni ya wananchi ni hatua ya kwanza  hivyo wananchi wajiandae na hatua zitakazofuata
tume ya mabadiliko ya katiba baada ya kumaliza kukusanya maoni katika wilaya za kakonko na kibondo sasa inaendelea na kazi hiyo ya kukusanya maoni ya wananchi katika wilaya ya kasulu mkoani kigoma MWISHO

No comments:

Post a Comment