KIBONDO.
Ubalozi wa Marekani Kupitia kituo cha Udhibiti wa Magonjwa (CDC ) wametoa msaada wa vifaa vya kufundishia na Kujifunza wenye thamani ya shilingi milioni 100sawa na dora 650 za kimarekani katika chuo cha ukunga Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma.
Akikabidhi Msaada huo, Mkurungenzi wa CDC Tanzania Dr. Michelle Rowland kwa mkuu wa Chuo hicho BI. Alfreda Ndunguru amesema msaada huo unalenga kuboresha mazingira ya kujisomea kwa wanachuo ili waweze kupata elimu bora kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.
Dr. Rowland amesema msaada huo ni utekelezaji wa mpango endelevu wa program ya watu wa marekani katika kupunguza tatizo la utoaji wa elimu duni kwa wanafunzi pamoja na kupunguza uhaba wa wataalamu wa afya nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Bi Alfreda Nduguru amepongeza hatua hiyo na kutoa wito kwa wahisani mbalimbali kuendelea kutoa misaada ya kuboresha elimu nchini kama chachu ya kuongeza idadi ya wataalamu na kupunguza tatizo la uhaba wa wafanyakazi wa kada mbalimbali. End’s
wanafunzi wa chuo cha uuguzi wilayani kibondo wakiimba kusherehesha katika hafla hiyo fupi |
mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto (kushoto )na mbunge bw Felix Mkosamali walikuwepo katika hafla hiyo ya kukabidhi msaada |
No comments:
Post a Comment