Wito umetolewa kwa wananchi wilayani kibondo mkoani kigoma
kuendelea kusalimisha siraha ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za watu
wanaomiliki siraha kinyume cha sheria
ili kuimarisha ulinzi na usalama miongoni mwa jamii
Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance
Mwamoto wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya mgambo katika kata ya Kitahana na
kuongeza kuwa raia wema wanaosalimisha siraha na wanaotoa taarifa za watu wanaomiliki siraha
hupewa motisha ya pesa isiyopungua shilingi elfu hamsini
Aidha bw Mwamoto amesema kuwa kwa yeyote anayetoa taarifa za
watu wanomiliki siraha kinyume cha sheria au kusalimisha siraha hawawezi
kuchukuliwa hatua yoyote ya kisheria badala yake atapewa motisha ili kusaidia
upatikanaji wa siraha nyingine Zaidi
Vijana wapatao 94 wote wa kiume wamemaliza mafunzo ya awali
ya mgambo kati ya 165 walionza mafunzo
hayo katika vijiji vya kibingo na Rusohoko kata ya Kitahana, mafunzo yaliyoanza lasmi tangu July 1 mwaka huu Ends
No comments:
Post a Comment