Pages

Wednesday, October 10, 2012

tume ya wizi wa shilingi milion mbili tarafa ya kifura yakamilisha ripoti

bi Jenisia Minani akiwa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya kibondo baada ya kupigwa na kunyang'anywa pesa shilingi milioni mbili na watu waliodhaniwa kuwa ni askari polisi (picha na james jovin )

KIBONDO


 

Tume  iliyoundwa na mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto kuchunguza sakata linalowahusu askari polisi wanne wa kituo cha Mkugwa tarafa ya kifura la kumpiga na kumpora mama mmoja pesa kiasi cha shilingi milioni mbili imemaliza kazi yake na kukabidhi lipoti hiyo


 

Akiongea na radio kwizera akiwa ofisini kwake  bw Mwamoto amesema kuwa tayari tume hiyo imemkabidhi lipoti hiyo ya uchunguzi juu yatukio hilo linalowahusu askari polisi lilitokea katika tarafa ya kifura septemba 17 mwaka huu


 

Pamoja na mambo mengine bw Mwamoto amesema kuwa kwa mujijbu wa taratibu ripoti hiyo ataiwakilisha kwa mkuu wa mkoa wa kigoma bw Salehe Issa Machibya  pamoja na mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa kigoma bw Fraizer Kashai kwa ajili ya kuisoma mbele ya wananchi wa tarafa ya kifura


 

Bi Jenisia Minani mwenye umri wa miaka 36 alivamiwa na kupigwa wakati akitoka dukani akielekea nyumbani  siku ya jumatatu septemba 17 usiku wa kuamkia jumanne hali iliyopelekea  kulazwa katika hospitali ya wilaya ya kibondo  na kwamba alinyang’anywa pesa kiasi cha shilingi million mbili pamoja na simu ya mkononi na watu waliohisiwa kuwa ni askari polisi wa kituo cha Mkugwa tarafa ya kifura  MWISH O

No comments:

Post a Comment