KIBONDO
Mkuu wa wilaya ya kibondo mkoani kigoma bw Venance Mwamoto
ameunda kamati ya amani inayohusisha viongozi wa dini za kiisilamu na kikiristo
,vyama vya siasa pamoja na viongozi wa serikali ili kutokomeza uvunjifu wa
amani unaofanywa na wahalifu wanaotumia mgongo wa madhehebu mbali mbali
Katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa vijana
wilayani kibondo wajumbe 17 wamechaguliwa kuongoza kamati hiyo ambapo wajumbe
hao wametoka katika mathehebu mbali mbali ya kikiristo na kiislamu pamoja na
vyama vya siasa
Mkuu wa wilaya ya kibondo bw Mwamoto amesema kuwa kamati
hiyo ya amani itasaidia kutatua kero mbali mbali zinazoanzishwa na watu binafsi
huku wakitumia mgongo wa dini au dhehebu Fulani na kusababisha vurugu
zisizokuwa na msingi miongoni mwa jamii
Akiongea katika mkutano huo wa kuchagua kamati ya amani bw
Mauld Juma ambaye ni mkazi wa kibondo mjini ameshauri kamati hiyo ihakikishe
makosa yanayofanywa na waumini wa kikirosto au kiisilamu wanayabeba wao wenyewe
na si kuyageuza ya kikundi au dini Fulani
Kamati hiyo ya amani imeungwa mkono na viongozi wa madhehebu
hayo ya kikiristo na kiislamu na kwamba imeundwa ili kulinda amani iliyopo
wilayani hapa na kuzuia fujo zinazoweza
kutokea ambapo siku za hivi karibuni kumekuwa kukitokea fujo zinazotokana na
visa vya kidini MWISHO
No comments:
Post a Comment