MTOTO Husuna Ramadhani (10), anayesoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Msiliembe, iliyopo Wilaya ya Uyui, mkoani Tabora, amekufa hapo hapo baada ya kupiga na radi ambayo pia iliwajeruhi wanafunzi wengine 23 ambao wamelezwa Hospital ya Mkoa Kitete kwa matibabu zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Edward Bukombe, alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni, katika Kijiji cha Msiliembe, Kata ya Mabama, saa nane mchana shuleni hapo.
Alisema mtoto huyo alifariki muda mfupi baada ya kupigwa na radi akiwa na wenzake darasani wakati mvua ikinyesha.
Kamanda Bukombe alisema mvua hiyo iliambatana na radi ambapo wanafunzi wa darasa la tatu na nne, wote walikaa katika chumba kimoja cha darasa wakiendelea kujisomea ndipo radi ilipopiga na kusabisha kifo hicho.
“Watoto wengene 23 waliuokuwepo katika darasa hilo, nao walipata madhara lakini watoto watano waliathirika zaidi na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Kitete,” alisema.
Aliwataja watoto waliolazwa kuwa ni Bundala Juma (10) anayesoma darasa la nne ambaye macho yake hayaoni vizuri, Hamisi Mashaka (10), anayesoma darasa la tatu, Cresesia Simon (12) na Kwangu Luone (12), ambao wote wanasoma darasa la nne na Zaituni Ally (10), anayesoma darasa tatu.
Alisema watoto hao wanaendelea na matibabu hospitalini hapo na kuwataka walimu kuakikisha wanafunzi wanaingia darasani mara mvua zinapoanza kunyesha....
No comments:
Post a Comment