meneja wa NMB kanda ya magharibi bw Manase Kituntu akikabidhi msaada wa magodoro kwa mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto |
Msahada huo ni pamoja na Magodoro 35 yenye thamani ya tsh million 2,975,00 kwa ajili wajawazito wa hospitali hiyo na Vyandarua 50 vyenye thamani ya tsh laki 500,000 kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa maralia kwa watoto wadogo
Akikabidhi msahada huo, kaimu meneja wa NMB kanda ya magharibi Bw Manase Kitundu kwa mkuu wa wilaya ya Kibondo, Bw Venance Mwamoto amesema msahada huo, unalenga kuunga mkono jitiahada za serikali katika kupambana na changamoto za upatiakanaji wa huduma bora za afya kwa wagonjwa
Kitundu alisema kuwa, pamoja na banki hiyo na kuunga mkono juhudi za serikali imefanya hivyo ilikuwajali wateja wake ili na wao waweze kujisikia kuwa wana banki inayo wajali
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kibondo Bw Venance Mwamoto amewapongeza NMB kwa hatua hiyo, na kutoa wito kwa wadau wengine kujitolea na kutoa misahada katika hospitali hiyo kwani inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa vifaa tiba na madawa
Nae Mganga mkuu wa wilaya hiyo, Bw Emmanuel Mwasulama aliishukuru Banki hiyo kwa kuamua kutoa msahada katika hospitali hiyo na kusema hakika pamoja na mambo mengine matatizo yatakuwa yamepungua kwakuwa wanayo wodi ya wajawazito ambayo ujenzi wake ulikuwa umekalika na ilikuwa na upungufu wa vitanda na magodoro. Mwisho
No comments:
Post a Comment