Pages

Monday, November 12, 2012

mbunge wa jimbo la muhambwe aahidi vitabu tani saba kwa shule mbali mbali za sekondari na msingi



mbunge wa jimbo la muhambwe wilayani kibondo bw Felix Mkosamali (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kushoto ni mwandishi wa habari James Jovin
Shule mbali mbali za sekondari na msingi zinategemea kunufaika na vitabu laki moja ikiwa ni mpango wa mbunge wa jimbo la muhambwe mkoani kigoma  wa kukuza kiwango cha elimu wilayani hapa ikiwa ni sambamba na kuweka motisha kwa walimu kuvutiwa kufundisha katika jimbo hilo

Akiongea na radio kwizera akiwa ofisini kwake mbunge wa jimbo la muhambwe bw Felix Mkosamali ameyasema hayo na kuongeza kuwa vitabu hivyo vimepatikana kwa msaada wa mashirika mbali mbali yasiyo ya kiserikali

Aidha pamoja na mambo mengine amesema kuwa shirika la twaweza pekee limefanikisha kupatikana kwa vitabu elfu alobaini na kwamba zoezi lililobaki ni kuvisafirisha kutoka dar es salaam mpaka wilayni kibondo kwa ajili ya kuvisambaza

Amesema kuwa anamkakati wa kuboresha elimu katika wilaya ya kibondo ambapo mbaka hivi sasa kuna vitabu laki moja ambavyo vimepatikana kutoka katika mashilika mbali mbali na kwamba ifikapo mwaka kesho vitabu hivyo vitakuwa tayari vimesambazwa katika shule mbali mbali za msingi na sekondari wilayani kibondo


Amesesema kuwa atahakikisha vitabu hivyo vinawafikia walengwa kabla ya January mwaka kesho ili wanafunzi watakapoanza muhula mpya wa masomo basi waanze wakiwa na vitabu hivyo vitakavyosaidia kwa kiasi kikubwa kuinua kiwango cha elimu

Aidha bw Mkosamali amesema kuwa katika kuhakikisha elimu inapewa kipaumbele amepanga kuvutia walimu kuja kufundisha katika jimbo la muhambwe ambapo pamoja na mambo mengine atahakikisha kila mwalimu mpya anapatiwa godoro na kitanda kama motisha  ikiwa ni pamoja na kila shule kupatiwa komputa 10 kabla ya uchaguzi ujao wa mwaka 2015 MWISHO

No comments:

Post a Comment