Mkazi wa kata ya mabamba wilayani kibondo mkoani kigoma
amehukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani baada ya kukili kosa la kukutwa na pombe haramu aina ya gongo kiasi
cha lita 500 yenye thamani ya shilingi laki saba na nusu
Mbele ya hakimu mkazi, mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya
kibondo bw Erick Marley mwendesha Mashitaka wa polisi bw Peter Makala amemtaja
mtu huyo kuwa ni Pius John mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa kata ya mabamba
Aidha bw Makala amesema kuwa usiku wa kuamkia leo February
25 mwaka huu kulipatikana taarifa za siri kuwa bw John ana stoo kubwa ya pombe
hiyo na baada ya polisi kupata taarifa hizo mkuu wa polisi tarafa ya mabamba bw
Fortunatus Rugumamu akishirikiana na serikali ya kijiji walifanya upekuzi na
kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa na pombe hiyo haramu ikiwa kwenye vyombo
mbali mbali kama madumu , ndoo na diaba
Baada ya kukamatwa bw pius John amehojiwa na kukili kuwa
pombe hiyo ni mali yake na alikuwa akiuza yeye mwenyewe mbele ya uongozi wa serikali ya kijiji na
polisi lakini pia mahakamani
Aidha baada ya mtuhumiwa kukili kosa Mwendesha mashitaka wa
polisi bw piter Makala ameiomba mahakama impe adhabu kali mtuhumiwa kwa kuwa
pombe hiyo huangamiza maisha ya watu wengi hapa nchini na kupunguza nguvu kazi
ya taifa hivyo adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa watu wengine wanaoshughulika na
kazi hiyo
Mahakama ya wilaya ya kibondo ikiongozwa na hakimu mkazi
mfawidhi bw Erick Marleye imemhukumu bw Pius John Kutumikia kifungo cha miaka
mitano gerezani baada ya kukili kutenda kosa hilo ili iwe fundisho kwa watu wengine
wanaojihusisha na biashara haramu ya kuuza pombe zilizopigwa marufuku na
serikali
Baada ya kutoa hukumu hiyo hakimu maley ameagiza pombe hiyo
haramu iteketezwe na jeshi la polisi chini ya usimamizi wa mkuu wa upelelezi wa
jeshi la polisi wilaya ya kibondo bw Twaha Rule na taarifa ya uteketezwaji wa
pombe hiyo haramu irudishwe mahakamani
No comments:
Post a Comment