KIBONDO
Idara ya elimu wilayani kibondo mkoani kigoma imejipanga kuhakikisha tatizo la wanafunzi kuchora vikatuni kwenye mitihani yao halijitokezi tena kwa kuzingatia taratibu na kanunzi zote zinazohusu mitihani inayotolewa na baraza la mitihani
Kauli hiyo imetolewa na makamu afisa elimu shule za msingi wilayani kibondo bw Mabeyo . S . Bujimu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akiwa ofisni kwake
Bw Bujimu pamoja na mambo mengine amesema kuwa tatizo hilo la kuchora vikatuni kwenye mtihani wa darasa la saba mwaka jana lilitokana na wasimamizi wa mtihani huo kutokuwa makini hivyo mwaka huu tayari maelekezo yametolewa kwa wasimamizi
Amesema kuwa kwa msimamizi yeyote atakaye enda kinyume na maelekezo ikiwa ni pamoja na kuvunja kanuni za mitihani hiyo atachukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa tayari wasimamizi wote wa mitihani hiyo wamepewa maelekezo ambapo pia amekili kuwepo kwa watahiniwa wasio jua kusoma na kuandika
Aidha kaimu afisa elimu huyo amewataka Wazazi na walezi kutowashawishi watoto wao kufanya vibaya mitihani pamoja na kuchora chora vitu visivyo eleweka kwa kisingizio cha kukosa karo ya kuwasomesha watoto hao kwa kuwa elimu ndio ulithi pekee unaoweza kuwakomboa na janga la umasikini
ameendelea kwa kusema kuwa mitihani yiyo ya kumaliza elimu ya msingi kwa mara ya kwanza itafanyika kwa kutumia teknolojia mpya ya optical mark reader (OMR) ambapo watahiniwa watatumia fomu maalum za OMR kujibia mitihani na majibu yao yatasahihishwa kwa kutumia komputa
bw BUJIMU Amesema kuwa maandalizi yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoj na mafunzo maalum kwa ajili ya matumizi ya fomu za OMR yamefanyika kwa lengo la kuwaandaa watahiniwa, wasimamizi pamoja na viongozi wa elimu katika ngazi mbali mbali ili waweze kutumia ipasavyo teknolojia hiyo
Jumla ya wanafunzi elfu saba na alobaini na tano (7045) wamesajiliwa kufanya mtihani ya kumaliza elimu ya msingi wilayani kibondo itakayofanyika kuanzia kesho jumatano septemba 19 na 20 kote nchini
No comments:
Post a Comment