Mechi
ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya Stand United na Kanembwa JKT
iliyochezwa Novemba 2 mwaka huu Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na
kuvunjika, sasa itarudiwa Februari 1 mwakani.
Uamuzi
huo umefanya na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake
kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine
ilipitia ripoti za mchezo huo uliovunika dakika ya 87.
TPLB
imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa mwamuzi Peter Mjaya
alitoa taarifa ambazo si sahihi kuhusu mechi hiyo. Mjaya ameondolewa
kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na FDL.
Mechi hiyo itarudiwa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo timu zote zimetumiwa uamuzi huo kwa maandishi.
Vilevile
wachezaji tisa wa Kanembwa JKT waliompiga mwamuzi katika mechi hiyo
suala lao linapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa ajili ya hatua zaidi
kwa mujibu wa Ibara ya 27(g)(3) ya Kanuni za FDL.
Wachezaji
hao ni Abdallah Mgonja, Baliki Abdul, Mbeke Mbeke, Mkuba Clement,
Mrisho Musa, Mtilakigwa Hussein, Nteze Raymond, Philo Ndonde na Uhuru
Mwambungu.
No comments:
Post a Comment