Mtoto anayekadiliwa kuwa na umri wa miezi sita amefariki
dunia baada ya kulaliwa na wazazi wake wanaoishi katika kitongoji cha boma
wilayani kibondo mkoani kigoma ambapo
inasemekana wazazi hao walikuwa wamelewa
Mwenyekiti wa kitongoji cha Boma bw Nuhu Kasiga amesema kuwa
baba wa mtoto huyo bw nshima buguru
ambaye nae alikuwa amelewa baada ya
kugundua kuwa mtoto amefariki majira ya saa 10 za usiku aliamka na kwenda kutoa taarifa kwa mwenyekiti huyo kwamba mkewe aitwaye mary
Antony amelalia mtoto akiwa amelewa na kusababisha kifo chake
Amesema kuwa hatua za kipolisi zimefanyika ambapo mwili wa
mtoto huyo ulichukuliwa na kupelekwa hospitali ya wilaya ya kibondo na mama wa
mtoto huyo bi Mary Antony anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano Zaidi
kuhusu tukio hilo la kusikitisha
Katika tukio linguine ni kwamba Mwanamke mkazi wa kata ya
Busunzu wilayani kibondo amefariki dunia baada ya kupigwa na radi katika nyumba
ya mkazi wa kitongoji cha kolimba alipokuwa amejikinga mvua wakati akitokea sokoni kijiji cha Nyakwi mwishoni mwa wiki iliyopita
Kaimu afisa mtendaji wa kata ya Busunzu bw Shabani Mahamud
Ruhinda amemtaja mwanamke huyo kuwa ni bi Salome Malora Mahangabili mwenye umri
wa miaka 50 mkaziwa kitongoji cha
mandela kata ya Busunzu wilayani kibondo
Bw Ruhinda amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi September
19 majira ya saa saba mchana ambapo maama huyo baada ya mvua kunyesha aliamua
kujikinga mvua kwa bw Godwin Ntambala wa kitongoji cha kolimba ndipo mauti
yakamkuta baada ya kupigwa na radi
Amesema kuwa baada ya mvua kupungua watu wengine waliokuwa
wamejikinga mvua pamoja katika nyumba hiyo walimuita ili waweze kuondoka na
alipofika mlangoni alipigwa na radi na kufariki dunia papo hapo na kwamba kifo
hicho hakijahusishwa na Imani zozote za kishirikina ENDS
No comments:
Post a Comment