Pages

Wednesday, October 8, 2014

WAUGUZI WAWILI NYAMAGANA WAFIKISHWA KIZIMBANI

Na Johnson James, Mwanza
WAUGUZI wawili wa Hospitali ya Butimba  Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza waliotambulika kwa majina ya Joyce mongo na Merystella Wilfred wakazi wa jijini hapa  wamepandishwa kizimbani  kwa tuhuma za kuomba na kupokea  rushwa kwa aliyekuwa mgonjwa Amina steven (sasa alishapona ) pamoja na kumuondolea  matone maji ya dawa maarufu kama dripu baada ya kumfanyia upasuaji wa kujifungua (operation).

Akiwasomea shitaka la kwanza mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nyamagana mkoa wa Mwanza  Chrescencia Mushi,  Wakili wa  jamhuri kwaniaba ya  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mwema Mella  alisema watuhumiwa Joyce Mongu na Marystela Winfred wote wakiwa wauguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana, walitenda kosa hilo Machi 12, mwaka huu.

Wakili  Mella, alisema wauguzi hao huku wakitambua kuwa wao ni watumishi wa serikali  kwa pamoja  waliomba rushwa ya Sh 50,000 kwa Rukia Daudi ambaye ni mzazi wa Amina Steven kama kishawishi cha kumuandaa mgonjwa kwa ajili ya upasuaji wa kujifungua kinyume na taratibu za mwajiri wake.

Katika shtaka la pili linalomkabili mtuhumiwa Marystela Winfred akiwa muuguzi katika hospitali hiyo ya Butimba Nyamagana, Machi 12 mwaka huu alidaiwa kupokea Sh 50,000 kutoka kwa Rukia Daudi kama kishawishi ili amfanyie binti yake Amina Steven upasuaji kwa ajili ya kujifungua.

Hata hivyo mahakama ilianza kusikiliza kesi hiyo ambapo upande wa jamhuri ulianza kuleta mashahidi wake ili kuthibitisha mashitaka hayo ambapo shahidi wa kwanza wa jamhuri  Rukia Daudi ambaye ni mama mzazi wa Amina alitoa ushahidi wake mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya na kueleza ushahidi wake ambapo alisema kuwa ni kweli tarehe 12 marchi mwaka huu  watuhumiwa kwa pamoja walimuomba  kiasi cha shilingi 50000 ili wamhudumie Amina baada ya kufanyiwa upasuaji  na asipofanya hivyo basi Amina ataweza kupoteza maisha kwakua watamuondolea dripu,  baada ya Rukia kupata taarifa  hizo aliamua kwenda kukopa kiasi hicho cha pesa iliawezekutoa na mwanaye (Amina) awezekupatiwa huduma za matibabu na akapata fedha hizo na kuzikabidhi kwa watuhumiwa ambao ni manesi wa hospitali ya Wilaya ya  Nyamagana.
Naye shahidi wa pili wa jamhuri  Amina Steven alitoa ushahidi wake mbele ya hakimu mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Nyamagana kwa kusema kuwa, nikweli tarehe 12 machi alikuwa hospitali ya wilaya ya Nyamagana akiwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji ndipo alipochomolewa dripu na na Nesi Joyce Mongo na kuelezwa kuwa kunapesa ametumwa mama yako yaani Rukia Daudi na kukurudishia hii dripu mpaka mama yako alete kiasi hicho cha pesa, nilikaa bilakupatiwa huduma yoyote kwa muda wa masaa matatu ndipo mama yangu akawa amepata kiasi hicho cha pesa ndipo nikarudishiwa dripu na kuendelea kupata huduma kama kawaida alisema’’ Amina 

Kwa upande wake Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza, Mbengwa Kasomambuto akitoa ufafanuzi wa watuhumiwa kuomba na kupokea rushwa  kwa wauguzi hao, alisema mnamo Machi 11 mwaka huu muuguzi Joyce alifika wodini alipokuwa amelazwa Amina Steven kwa ajili ya kumfanyia vipimo na baadaye saa 10 usiku alimuagiza muuguzi wa zamu kuomba fedha kwa mgonjwa ili aweze kumhudumiwa.

Machi 12 mwaka huu baada ya ndugu wa mgonjwa kupigiwa simu na wakiombwa Sh 50,000 ili aweze kufanyiwa upasuaji, ndugu wa mgonjwa huyo alifika hospitalini hapo na kwa kuwa hakuwa na kiasi hicho aliomba kuweka simu yake rehani lakini Joyce ambaye ni muuguzi alikataa na kusisitiza kuwa wanahitaji fedha.

Ndugu huyo (jina linahifadhiwa) baada ya kukwama kutoa fedha alishuhudia mgonjwa wake akitolewa dripu kwa maelezo kwamba mpaka atakapolipa kiasi hicho cha fedha alichoombwa, na baadaye kufanikiwa kupata kiasi hicho kwa mkopo na kumkabidhi nesi huyo aliyemrejeshea mgonjwa dripu, lakini muuguzi huyo alipoombwa stakabadhi ya malipo aligoma kutoa.
Kesi hiyo imeahirishwa na inatarajia kuendelea tena hapo kesho kwa mijibu wa hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya nyamagan

No comments:

Post a Comment