mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto (kushoto) akiangalia dodoso zilizochanwa na makarani wa sensa ya watu na makazi (picha na james jovin )
KIBONDO
Watu wawili makarani wa sensa wilayani kibondo mkoani kigoma
wanashikiliwa na jeshi la polisi wakituhumiwa kuchana dodoso za sensa ya watu
na makazi inayoendelea nchi nzima
Jeshi la polisi limesema kuwa makarani hao ni pamoja na bw
Elisha Helmsns claudias ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu dodoma pamoja na Fredrick Mhalafu mkazi wa
kibondo mjini
Jeshi la polisi wilayani hapa limesema kuwa bw Elisha
Helmans alichana dodoso alizokuwa ameshika bw Fredrick Mhalafu katika kituo
walichopangiwa kifura shule ya msingi katika tarafa ya kifura kata ya Busunzu
wilayani kibondo
Tukio hilo limetokea jumatatu
august 26 huko kifura wakati vijana hao pamoja na makarani wenzao wakijaribu
kushinikiza kulipwa posho zao baada ya kuletewa posho nusu kinyume na
makubaliano yao
Mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto ambaye pia
aliongozana na mkuu wa jeshi la polisi bw Marko Joshua amewataka makarani
kuendelea na zoezi la sensa na kuwahakikishia kuwa watalipwa posho yao yote
Makarani hao wa sensa ya watu na makazi wanashikiliwa na
jeshi la polisi wilayani hapa kwa uchunguzi zaidi wa tukio hilo ambapo pia
limewataka makarani kuendelea na zoezi la sensa na kutochana madodoso kwa kuwa
ni kosa kisheria MWISHO
No comments:
Post a Comment