Pages

Sunday, October 21, 2012

halmashauri wilayani kibondo yapata pigo muuguzi daraja la pili afariki dunia

marehemu Rwechungula paul aliyekuwa muuguzi daraja la pili katika zahanati iliyoko kijiji cha kibuye wilayani kibondo (picha na Awino Fransis )

Kibondo

Wananchi wa kijijij cha kibuye wilayani kibondo wametishia kuhama kijiji hicho baada ya kifo cha aliyekuwa muuguzi wa zahanati ya kijiji hicho kilichotokea baada ya kuzama katika mto malagarasi alipokuwa akiogerea wakimtuhumu bw Raulent  ntatinya kuwa alihusika na kifo hicho kwa kuwa alimtishia marehemu kuwa atamuua kabala ya kutokea kwa tukio hilo

Jeshi la polisi wilayani kibondo limesema kuwa tukio hilo limetokea jumatano ya wiki iliyopita October 17 na kwamba waliofariki ni Rwechungula Paul mwenye umri wa miaka 22 ambaye alikuwa muuguzi daraja la pili katika kituo cha afya mkibuye pamoja na Habili Kitika mkazi wa kijiji hicho

Katibu wa idara ya afya wilayani kibondo bw Awino Fransis ambaye alifika katika eneo la tukio amesema kuwa malehemu alienda katika mto huo akiwa na marafiki zake watatu ambao wote hawajui kuogelea kwa nia ya kuangalia mto huo ndipo marehemu akajaribu kuogelea hata hivyo hakufahamu sehemu hiyo kama ilikuwa na kina kilefu
Amesema kuwa marehemu alizama ndipo kijana aliyeona tukio hilo ambaye kidogo ni mzoefu wa kuogelea alijaribu kuingia kumuokoa bw Rwechungula kwa bahati mbaya alimkumbatia kwa nguvu ndipo kijana huyo akashindwa kumuokoa wakafariki wote kwa pamoja katika mto huo
Vijana watatu waliokuwa pamoja na marehemu hawakuwa na uzoefu na masuala ya kuogelea hivyo waliangalia tu kama sinema baada ya tukio hilo walikimbia kutoa taarifa kwa viongozi wa kijiji majira ya saaa moja jioni miili ya marehemu ikaopolewa
Mwili wa marehemu Rwechungula paul tayari umesafirishwa mpaka kwao Wilayani karagwe mkoani kagera kwa ajili ya mazishi na kwamba kijana aliyejaribu kuogelea tayari amezikwa kijijni kwake Kibuye

Sakata la kifo cha vijana hao wawili limeendelea kushika sura mpya baada ya wananchi wa kijiji cha kibuye kumtilia mashaka bw Laurent Ntatinya  na kumtaka ahame katika kijiji hicho baada ya walimu pamoja na wauguzi kutaka kuhama  kitu kilichopelekea mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto  pamoja na mkuu wa jeshi la polisi bw Joshua Marko  kufika kijijini hapo kwa ajili ya kusuruhisha suala hilo

Afisa mtendaji wa kijiji hicho bw Ayubu Gabriel amesema kuwa kabla ya vijana hao kufariki bw Ntatinya alimtishia muuguzi huyo kuwa atamuua na kwamba amekuwa akitishia wananchi kijijini hapo ambapo anaposema jambo ni lazima litokee
Aidha kabla ya kifo hicho zilikutwa dawa za kienyeji katika kufuri la mlango wa zahanati ya kijiji cha mkabuye ambapo marehemu alikuwa akifanya kazi na kwamba tukio hilo lilitokea baada ya bw Ntatinya kumtaka bw Rwechungula ampe dawa anazotaka yeye bila kufuata utaratibu

Mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto ameagiza bw Ntatinya akamatwe au aende yeye mwenyewe katika kituo cha polisi kibondo baada ya kukaa na wazee wa kijiji hicho cha kibuye na kusema kuwa kama mtu huyo hata hama kijijijni hapo basi watahama wao  MWISHO

maji ya mto malagaras sehemu marehemu alipokuwa akiogelea kabla ya kifo chake 




zahanati ya kijiji cha kibuye alipokuwa akifanya kazi marehemu Rwechungura paul

wazazi wa kijana aliyetaka kumuokoa marehemu rwechungula ,inasemekana kijana huyo ambaye hata hivyo alifariki alikuwa mtoto pekee katika familia hiyo (picha zote kwa hisani ya Awino Fransis)
 REST IN PIECE RWECHUNGURA & HABILI

No comments:

Post a Comment