profesa Ibrahimu Haruna Lipumba mwenyekiti chama cha wananchi CUF |
Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF taifa Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba amesema kuwa ni vema kwa watu wanaovunja sheria wawe raia wa kawaida ,kiongozi au askari kuchukuliwa sheria kama inavyopaswa ili kuleta imani kwa wananchi na kudumisha amani kote nchini
Profesa lipumba ametoa rai hiyo katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa vijana baada ya kupewa taarifa kuwa miezi kadhaa iliyopita askari wanne wa kituo cha kifura walituhumiwa kumpiga mama mmoja na kumnyanganya pesa kiasi cha milioni mbili
Aidha profesa Ibrahimu Lipumba ameshangazwa na kitendo cha maaskari polisi hao wanne waliotuhumiwa kumpiga na kumpora mama mmoja pesa shilingi milioni mbili katika tarafa ya kifura kutochukuliwa hatua za kisheria na badala yake wamehamishwa vituo vya kazi
Pamoja na mambo mengine amesema kuwa jambazi anapokuwa amekamatwa anatakiwa afikishwe mahakamani ikiwa ni pamoja na kuondolewa kazini ili sheria iweze kuchukua mkondo wake kwa kuwa sheria ni kama msumeno hukata pande zote
Aidha profesa lipumba ameshangazwa na kitendo cha mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto kuunda tume ya kuchunguza sakata hilo ambapo hata hivyo majibu ya uchunguzi huo bado hayajatolewa mpaka hivi sasa
Bi Jenisia Minani mwenye umri wa miaka 36 alivamiwa na kupigwa wakati akitoka dukani akielekea nyumbani siku ya jumatatu septemba 17 usiku wa kuamkia jumanne hali iliyopelekea kulazwa katika hospitali ya wilaya ya kibondo na kwamba alinyang’anywa pesa kiasi cha shilingi million mbili pamoja na simu ya mkononi na watu waliohisiwa kuwa ni askari polisi wa kituo cha Mkugwa tarafa ya kifura wilayani Kibondo MWISHO
No comments:
Post a Comment