Mamlaka ya chakula na dawa TFDA imefunga machinjio ya nyama wilayani kibondo baada ya machinjio ya muda iliyoko katika jengo la kalakana lililopo karibu na stand mpya ya mabasi kuonekana kuwa na upungufu wa baadhi ya mahitaji ya muhimu kama choo na maji
Akiongea na waandishi wa habari afisa afya wa wilaya ya kibondo BW Joab Kabetero amesema kuwa mamlaka ya chakula na dawa imeamua kufunga machinjio hiyo ya nyama wilayani hapa kutokana na sababu mbali mbali ambazo zinaweza kuhatarisha afya ya mlaji ikiwemo kukosekana kwa huduma ya maji ambayo hutumika kusafishia nyama
Aidha bw Kabetero amezitaja sababu zilizopelekea machinjio hiyo kufungwa na mamlaka hiyo ya chakula na dawa TFDA kuwa ni pamoja na kutokuwa na choo kwa ajili ya wachinjaji kujisaidia na maji kwa ajili ya kusafishia nyama kama inavyopaswa pia amewataka walaji kuwa wavumilivu kwa wakati huu ambao halmashauri ya wilaya inakamilisha ujenzi wa machinjio mpya itakayokidhi mahitaji na afya za walaji
Aidha kaimu mwenyekiti wa wafanyabiashara wilayani kibondo bw Gervaz Mpagaze amesema kuwa uzembe wa halmashauri ya wilaya ndio uliopekekea kutokea kwa matatizo hayo kwa kuwa walipaswa kuhakikisha choo kinakuwepo pamoja na maji kwa kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wakitoa ushuru kama inavyopaswa
Aidha mmoja wa wafanyabiashara wa mgahawa wilayani hapa bw Samson Kayabu amesema kuwa wameadhilika kwa kiasi kikubwa kutokana na tatizo hilo la ukosefu wa nyama na kwamba wateja wamepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa wengi hupendelea kula nyama
Machinjio iliyokuwa ikitumika kwa zaidi ya miaka 15 iliyopita ilifungwa kutokana na kutokuwa na huduma hizo muhimu kama za maji na choo , machinjio ya muda iliyokuwa imeanzishwa katika jengo lililokuwa la karakana ya magari nayo imefungwa kutokana na kutokuwa na huduma kama hizo pia machinjio mpya iliyojengwa imeshindikana kutumika kutokana na kwamba ilijengwa chini ya kiwango na kwamba kwa hivi sasa imejaaa maji kutokana na kutitia katika eneo ilipojengwa
Swali ni kwamba kama wachinjaji na wafanyabiashara hao wa nyama wanatoa ushuru kama inavyopaswa nani anaepaswa kujenga choo na kuhakikisha miundo mbinu ya maji inakuwepo……………………………….………. Tafakari chukua hatua MWISHO
No comments:
Post a Comment