Pages

Thursday, November 1, 2012

matumizi mabaya ya madaraka yamshusha cheo afisa elimu kibondo

Baraza la Madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma limemvua madaraka ya Kuwa Mkuu wa Idara ya shule za Msingi Bw.Bulingama Nyalinga na kubaki kama mwalimu wa kawaida baada ya tume iliyoundwa kumchunguza ukiukwaji wa taratibu za utumishi   kubaini kuwa anamakosa.

 mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Bw. Juma Maganga ameyasema hayo  katika kikao cha baraza la madiwani wakati akitoa taarifa ya tume ya  uchunguzi iliyoundwa kumchunguza aliyekuwa Afisa wa idara ya elimu ya shule za msingi Bw. Bulingama Nyalinga.

Bw. Maganga amesema Nyalinga amebainika kuwa na makosa matatu likiwemo la kuzolotesha na kuporomoka kwa elimu wilayani kibondo sambamba na mahusiano mabaya baina ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka akiwa afisa elimu wa wilaya  .

Aidha amesema Bw. Bulingama Nyalinga anatakiwa kukata rufaa ya kupinga maamuzi hayo ya baraza la madiwani ndani ya siku 45 endapo hata lidhika na maamuzi hayo.

Hata hivyo ametoa wito kwa wakuu wa idara na wafanyakazi wa halmashauri kufuata kanuni na taratibu za utumishi bora katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kuepuka migongano na migogoro wawapo kazini. End’s

No comments:

Post a Comment