Kesi 45 kati ya 70 zilizofikishwa kwenye dawati la utatuzi wa migogoro ya ardhi lililoanzishwa na mkuu wa wilaya ya kibondo zimemalizika baada ya kushughulikiwa na dawati hilo ikiwa ni harakati za kutatua migogoro mbali mbali ya ardhi
Akiongea na waandishi wa habari mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance mwamoto ameyasema hayo na kuongeza kuwa ameamua kuanzisha dawati hilo ili kusaidia wananchi wanao poteza haki zao za msingi hivyo kupelekea migogoro isiyoisha miongoni mwa jamii
Aidha bw Mwamoto amesema kuwa utendaji kazi wake mzuri wa kusikiliza kila mtu anayefika ofisini kwake umepelekea yeye kulaumiwa kuwa ameingilia mpaka shuhguli ambazo zingefanywa na balozi wa nyumba kumi
Bw Mwamoto amesema kuwa sambamba na hilo ameanzisha dawati la jinsia na malalamiko ambalo litakuwa likisaidia kutatua kesi mbali mbali ili kusaidia kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani ambazo zingemalizika bila kufika mbali zaidi
Katika hatua nyingine ni kwamba Mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto amefanya kazi ya kutambua vikundi mbali mbali kama wazee, vijana na walemavu ili kuwaanzishia mikakati mbali mbali ya kazi za kujitegemea ikiwa ni kwa maendeleo yao na kupunguza raslimali watu wasio na ajira
Aidha bw Mwamoto amesema kuwa tayari amevitambua vikundi hivyo na kwamba mipango mbali mbali ya kuhakikisha wanaendelea inaendelea na kwamba ni lazima kuwajengea mazingira ya kazi ili kuepuka kuwa tegemezi
Pamoja na mambo mengine bw Mwamoto amesema kuwa ili kuviwezesha vikundi hivyo kujitegemea ni bora kuvipatia vetendea kazi pamoja na kuwafundisha kazi mbali mbali za mikono kuliko kuwapa pesa ambazo huenda zikatumika vibaya
katika miezi mitano aliyokaa wilayani kibondo mkuu wa wilaya ya kibondo amesema kuwa amefanikiwa katika mambo mbali mbali ikiwemo kuweka uhusiano mzuri na mikoa ya nchi jirani ya Burundi ,kusogeza mpaka uliokuwa ndani ya nchi ya Tanzania pamoja na kutatua migogoro mbali mbali ya ardhi MWISHO
No comments:
Post a Comment