Halmashauri ya wilaya ya kibondo mkoani kigoma
imeidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 3 na milioni 347 katika mwaka wa fedha
2013/ 2014 kutoka serikali kuu na wahisani mbali mbali wa maendeleo kwa ajili
ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoko chini ya kamati ya elimu afya na
maji
Mwenyekiti wa kamati ya elimu afya na maji bw Ali Amini
Gwanko Mpondamali ameyasema hayo wakati akisoma taarifa ya kamati hiyo katika
baraza la madiwani lililoketi leo katika ukumbi wa vijana na kuongeza kuwa
fedha hizo ni sawa na asilimia 57.5 ya bajeti yote iliyoidhinishwa
Aidha bw Gwanko amesema kuwa halmashauri ilikuwa imebaki na
salio ishia kwa mwaka wa fedha 2012/2013 kiasi cha shilingi bilioni 3 na
milioni 525 hivyo pesa itakayotekeleza miradi mbali mbali katika kamati hiyo
kwa mwaka wa fedha 2013/2014 itakuwa zaidi ya shilingi bilioni 6
Amesema kuwa katika utekelezajaji wa miradi mbali mbali
kamati ya elimu, afya na maji kwa mwaka wa fedha uliopita ilikabiliwa na
changamoto mbali mbali ikiwemo kuchelewa kuanza kwa mfumo wa EPICA na hivyo
kushindwa kufanya malipo kwa wakandarasi wenye mitaji midogo hivyo kukwamisha
kazi
No comments:
Post a Comment