mkuu wa wilaya ya kibondo bw venance mwamoto akicheza na mlemavu asiyeona ikiwa ni moja wapo ya njia ya kuwapa furaha walemavu |
Wito umetolewa kwa serikali kuchukua hatua madhubuti ya
kutatua kero mbali mbali zinazowakabili watu wenye ulemavu ikiwemo kuhamasisha
wazazi kutowafungia watoto wenye ulemavu ndani
na kushindwa kuwapeleka shule kwa kisingizio cha kuchekwa ama kutengwa
na jamii
Wito huo umetolewa na mwenyekiti
wa chama cha walemavu wilayani kibondo bw Evalisto Ngalama wakati akizungumza
na kibondo moto na kuongeza kuwa ikiwa walamavu watawezeshwa
hasa kupewa mafunzo ya ufundi basi serikali itapunguza watu tegemezi kwa kiasi
kikubwa sana
Aidha bw Ngarama amesema kuwa serikali ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania inapaswa kuchukua hatua madhubuti ya kuwasaidia walemavu
ili kujenga jamii yenye usawa , upendo , mshikamano pamoja na amani
Bw Ngarama ameema kuwa jamii kwa kushirikiana na serikali,
taasisi binafsi inatakiwa kujenga miundombinu rafiki kwa walemavu
itakayowarahisishia kupata huduma muhimu za afya na elimu ili kuondokana na
adha wanayoipata pindi wanapohitaji huduma hizo. ENDS
No comments:
Post a Comment