bw Venance Mwamoto akisoma majina ya wazee wenye sifa za kupata mbolea hiyo |
KIBONDO
Mkuu wa wilaya ya kibondo bw Venance Mwamoto amegawa mifuko
78 ya mbolea aina ya Minjingu kwa wazee wapatao 164 wa kijiji cha Kibuye Kata
ya Kumsenga aliyoikamata mwaka jana
ikiwa kwenye harakati za kuvushwa nje ya nchi kwa njia za magendo
Bw Mwamoto amesema kuwa ameamua kutoa mbolea hiyo kwa wazee
wa kijiji cha Kibuye kwa kuwa ilikamatiwa kijijini hapo mwaka jana kabla ya
kuvushwa kwenda nchi jirani ya Burundi ikiwa ni kwa njia za magendo ‘’ nimeamua
kugawa mbolea hii kwa wazee kuwa kuwa wao kwanza hawana nguvu na itawasaidia
kuboresha mashamba yao na kuongeza kipatocha familia’’ alisema mwamoto
Bw Mwamoto amesema kuwa ameamua kugawa mifuko 74 kwa wazee
kisha kubakiza mifuko mingine minne ya mbolea hiyo kwa ajili ya ushahidi kwa
watu wa TAKUKURU pamoja na polisi kama itahitajika kufanya hivyo kwa upelelezi
Zaidi wa wahusika wa wizi wa mbolea hiyo
Bw Mwamoto amesema
kuwa alikamata mbolea hiyo mwaka jana mwezi wa katika kijiji cha Kibuye
kata kumsenga ikiwa kwenye harakati ya kuvushwa kwenda nchi jirani ya Burundi
kwa ajiri ya kuuzwa huko pamoja na kwamba mbolea hiyo ilitolewa kama ruzuku kwa
wananchi wa wilaya ya kibondo
Mmoja wa wazee hao bw Charles Ntambala amesema kuwa amefurahishwa
na zoezi hilo na kwamba litakomesha wizi wa mbolea ambao umekuwepo kwa muda
mrefu na kusababisha wanyonge kutopata haki yao ya msingi kutokana na kuuzwa
kwa matajiri wa nchi jirani ‘’ kama unavyojua ndugu mwandishi hapa ni mpakani
mbolea imekuwa ikifanyiwa magendo kwa muda mlefu sana na kusababisha sisi
tukose haki yetu ya msingi kutokana na mbolea kuongezeka bei maradufu kutona na
kuuzwa nje ya nchi namshukuru sana mkuu wa wilaya haijawahi kutokea tangu
niishi kijii hiki’’ alisema mzee huyo
Bw mwamoto amesema kuwa zoezi la ukamataji mbolea
inayofanyiwa magendo litakuw aendelevu ili kukomesha wizi huo unaosababisha
wananchi wakose haki yao ya msingi na kudumaza maendeleo kwa watanzania ENDS
No comments:
Post a Comment